Katiba mpya inayotokana na Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Warioba imeweka muundo wa serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya nchi washirika yaani Jamhuri ya Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika Rasimu hii ambayo ilikuja kujulikana kama Rasimu ya Katiba ya Wananchi (Rasimu ya Katiba - ya Warioba (PDF)) iliungwa mkono na wananchi walio wengi ingawa ilikuja kuhujumiwa katika Bunge la Katiba na kambi ya chama tawala CCM. Hata hivyo kiu ya watanzania bado ni kubwa ya kupata Katiba Mpya ya Wananchi wenye mfumo wa serikali tatu. Kikwazo moja kikubwa kilichoibuliwa hata kwenye Bunge la Katiba ni kutokuwepo kwa Tanganyika. Ingawa Katiba ya sasa imemeza Tanganyika lakini haina maana nchi mshirika Tanganyika haipo ila haina Katiba yake wala haijapewa hadhi sawa na Zanzibar ambayo ina serikali, mahakama na bunge lake (Katiba ya Zanzibar (PDF)). Kwa mujibu wa tume ya Mabadiliko ya Katiba na rasimu, hatua ambayo ingefuata baada ya kupitishwa kwa rasimu hii ingekuwa kutunga Katiba ya Tanganyika. Na hoja moja kubwa ya waliopinga rasimu hii ilikuwa kwamba katiba ya Tanganyika haipo. Hivyo basi sisi wananchi tumeamua kuandaa rasimu ya Katiba ya Tanganyika kama wazo ili tupate pa kuanzia na tuweze kuweka hadharani Tanzania tuitakayo yenye Tanganyika kama nchi mshirika kwa mujibu wa rasimu ya Warioba. Tukishakubaliana kuhusu Tanganyika basi hakuna kinachozuia Rasimu ya Katiba ya tume ya Warioba kufanyiwa kazi na kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rasimu hii ya Katiba ya Tanganyika ina sura 10 na imezingatia mawazo yaliyotolewa kwa tume iliyoongozwa na Jaji Warioba iliyotaka mamlaka irudishwe kwa wananchi kwa ngazi ya chini ya maamuzi. Hivyo kuna sura maalum ya UGATUZI inayorudisha mamlaka kwa wananchi hadi ngazi ya mtaa. Huu si mfumo wa sasa ambao umejificha chini ya TAMISEMI huku maamuzi na bajeti zote ni za serikali ya Muungano. Ugatuzi umefanyika katika sekta zote ikiwemo mahakama, utendaji na uwakilishi lakini hata katika masuala ya ulinzi na usalama, vyombo husika vimesogezwa karibu na wananchi. Haya ni mawazo na kama kawaida yanahitaji maboresho. Tunakaribisha watanganyika wote na wapenda haki kutoa maoni na kushiriki kikamilifu katika kuboresha rasimu hii ili mjadala uanze kuhusu Tanganyika na Tanzania Mpya tuitakayo.
Karibuni!

Tanganyika flag

Katiba Mpya ya Tanganyika

Sura ya 0

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
UTANGULIZI

Sisi Watu wa Jamhuri ya Tanganyika kwa:
KUTUMIA haki yetu ya asili na isiyoweza kuondolewa ya kuanzisha mfumo wa serikali, ambao utatuhakikishia sisi na vizazi vijavyo, jamii iliyojengwa juu ya misingi ya utu, uhuru, haki, heshima kwa wote, usawa, undugu, amani na haki ya kutafuta furaha;
KUHESHIMU ari ya kujenga na kukuza amani na umoja na watu wote wa Afrika na Ulimwengu;
KUWATAMBUA wale ambao walijitahidi kuleta uhuru na haki katika nchi yetu
TUMEDHAMIRIA KUWA:
. Katiba hii ndo mwongozo wa juu ya nchi na ni juu ya sheria nyingine zote;
· Msingi pekee wa mamlaka yote ya nchi yanatokana na wananchi wenyewe ;
TUMEAZIMIA KUWA NA:
· Serikali ambayo inatokana na wananchi, kwa ajili ya wananchi, na kuendeshwa na wananchi, na mihimili yote ya serikali inajitegemea na kudhibitiana ili kuhakikisha hakuna iliyo juu ya nyingine;
· Kanuni ya ushiriki wa umma ambapo utawala unashirikisha wananchi katika ngazi zote za serikali na maamuzi yote yanafanywa kwa pamoja;
·Msingi wa kidemokrasia ambayo inatambua na kulinda watu binafsi kutokana na ubabe ya walio wengi
· Utawala wa Sheria;
· Ulinzi na uhifadhi wa haki za kimsingi za binadamu na uhuru;
· Misingi ya usawa, kujitegemea na uzalendo;
NA KWA KUZINGATIA uzoefu wetu kupitia Uhuru wa Tanganyika, Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na umuhimu wa ushiriki kamili na wa wazi wa watu katika mchakato wa kuandika Katiba
TUNATUNGA, TUNAPITISHA NA KUTOA KATIBA HII KWA AJILI YETU NA KWA VIZAZI VYETU VIJAVYO WA NCHI YETU

(Hakuna ibara yaliyopatikana.)

Sura ya 1

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
MWANZO

JAMHURI, KATIBA NA WATU, URAIA

🔍 Tazama Ibara (Ibara 18 kutoka #1 hadi #18.)

Sura ya 2

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
HAKI ZA RAIA

Sehemu hii ina haki za msingi za raia ikiwemo haki za kiraia na kisiasa, haki za kijamii, kiuchumi, kitamaduni na za jumla. Inajumuisha matumizi, utekelezaji, na masharti ya haki.

🔍 Tazama Ibara (Ibara 36 kutoka #1 hadi #36.)

Sura ya 3

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
ARDHI NA MALIASILI

xxxxxxxxxxxxxxx

🔍 Tazama Ibara (Ibara 14 kutoka #1 hadi #14.)

Sura ya 4

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
SERIKALI YA TANGANYIKA

SERIKALI, RAIS NA MAKAMU WA RAIS

🔍 Tazama Ibara (Ibara 10 kutoka #1 hadi #10.)

Sura ya 5

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
BUNGE LA TANGANYIKA

MUUNDO NA MAMLAKA YA BUNGE, WABUNGE, UONGOZI WA BUNGE, TARATIBU ZA SHUGHULI ZA BUNGE LA KITAIFA

🔍 Tazama Ibara (Ibara 28 kutoka #1 hadi #28.)

Sura ya 6

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
MAHAKAMA

xxxxxxxxxxxxxxx

🔍 Tazama Ibara (Ibara 12 kutoka #1 hadi #12.)

Sura ya 7

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
UGATUZI

xxxxxxxxxxxxxxx

🔍 Tazama Ibara (Ibara 9 kutoka #1 hadi #9.)

Sura ya 8

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
TAASISI ZA KUJITEGEMEA

xxxxxxxxxxxxxxx

🔍 Tazama Ibara (Ibara 14 kutoka #1 hadi #14.)

Sura ya 9

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
USALAMA WA KITAIFA

xxxxxxxxxxxxxxx

🔍 Tazama Ibara (Ibara 9 kutoka #1 hadi #9.)

Sura ya 10

(Maoni 0 yamepatikana) ✏️ Ongeza Maoni
MASHARTI YA MPITO, MAREKEBISHO, NA REFERENDA

xxxxxxxxxxxxxxx

🔍 Tazama Ibara (Ibara 3 kutoka #1 hadi #3.)